Music theory is the study of the practices and possibilities of music. |
Nadharia ya muziki ni utafiti wa mfumo na uhuru wa muziki. |
Music theory is frequently concerned with describing how musicians and composers make music, including tuning systems and composition methods among other topics. |
Nadharia ya muziki mara kwa mara inahusika na kuelezea jinsi wanamuziki na watunzi wanavyotengeneza muziki, ikijumuisha mifumo ya kurekebisha na mbinu za utunzi miongoni mwa mada nyingine. |
Because of the ever-expanding conception of what constitutes music (see Definition of music), a more inclusive definition could be that music theory is the consideration of any sonic phenomena, including silence, as they relate to music. |
Kwa sababu ya dhana inayozidi kupanuka kuhusu kile kinachojumuisha muziki (ona maana ya muziki), maelezo yanayojumuisha zaidi ni kwamba nadharia ya muziki ni kule kuzingatia kwa matukio yoyote ya sauti, ikiwa ni pamoja na kimya, kama yanavyohusiana na muziki. |
This is not an absolute guideline; for example, the study of "music" in the Quadrivium liberal arts university curriculum that was common in medieval Europe was an abstract system of proportions that was carefully studied at a distance from actual musical practice. |
Huu sio mwongozo kamili; kwa mfano, somo la "muziki" katika mtaala wa chuo kikuu cha sanaa huria cha Quadrivium uliokuwa kawaida katika Ulaya ya zama za kati, ulikuwa ni mfumo dhahania wa uwiano ambao ulisomwa kwa makini mbali na mazoezi halisi ya muziki. |
However, this medieval discipline became the basis for tuning systems in later centuries, and it is generally included in modern scholarship on the history of music theory. |
Walakini, nidhamu hii ya zama za kati ikawa ni msingi wa mifumo ya kurekebisha katika karne za baadaye, na kwa ujumla inahusishwa katika usomi wa kisasa juu ya historia ya nadharia ya muziki. |
Music theory as a practical discipline encompasses the methods and concepts composers and other musicians use in creating music. |
Nadharia ya muziki kama taaluma inayotekelezwa inajumuisha mbinu na dhana zinazotumiwa na watunzi na wanamuziki wengine katika kuunda muziki. |
The development, preservation, and transmission of music theory in this sense may be found in oral and written music-making traditions, musical instruments, and other artifacts. |
Ukuzaji, uhifadhi, na uwasilishaji wa nadharia ya muziki, kwa dhana hii, inaweza kupatikana katika mila ya utunzi wa muziki wa mdomo, maandishi, ala za muziki na aina zingine. |
For example, ancient instruments from Mesopotamia, China, and prehistoric sites around the world reveal details about the music they produced and potentially something of the musical theory that might have been used by their makers (see History of music and Musical instrument). |
Kwa mfano, ala za kale kutoka Mesopotamia, Uchina, na tovuti za kihistoria duniani kote hufichua maelezo kuhusu miziki waliounda, na pengine uwepo wa nadharia ya muziki ambayo huenda ilitumiwa na watunzi wake (ona Historia ya muziki na ala ya Muziki). |
In ancient and living cultures around the world, the deep and long roots of music theory are clearly visible in instruments, oral traditions, and current music making. |
Katika tamaduni za zamani na zilizo hai ulimwenguni kote, mizizi mirefu na ya kina, ya nadharia ya muziki inaonekana wazi katika ala, mila za mdomo, na utengenezaji wa muziki wa sasa. |
Many cultures, at least as far back as ancient Mesopotamia and ancient China, have also considered music theory in more formal ways such as written treatises and music notation. |
Tamaduni nyingi, angalau za hapo awali kama Mesopotamia ya kale na Uchina wa kale, pia zimezingatia nadharia ya muziki kwa njia rasmi zaidi kama vile maandishi na nukuu za muziki. |
Practical and scholarly traditions overlap, as many practical treatises about music place themselves within a tradition of other treatises, which are cited regularly just as scholarly writing cites earlier research. |
Tamaduni za utekelezaji na za kielimu zinaingiliana, kwani maandishi mengi ya vitendo kuhusu muziki hujiweka ndani ya utamaduni wa mikataba mingine, ambayo inatajwa mara kwa mara. Kama vile uandishi wa kitaalamu unavyonukuu kuhusu utafiti huo mbeleni. |